Kwa Mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Sheikh Mkuu wa Jumuiya ya Shia Ithnaasharia Tanzania Samaahat Sheikh Hemedi Jalala Mwakindenge, jana jumamosi akiambatana na jopo zima la Jumuiya ya Shia Ithnaasharia Tanzania (TIC), pamoja na walimu na wanafunzi wa Hawza ya Imaam Sw'adiq (as), walihudhuria kwenye Hauli ya Hayati Sheikh Abdallah Seifu Linganaweka (ra), iliyofanyika kijijini kwake Lindi.
Akizungumza na wakazi wa kijiji cha Mnang’ole Lindi, katika Hauli hiyo ambayo iliambatana na hafla ya Maulid ya Mtume Muhammad (s.a.w.w), Sheikh Jalala alielezea historia ya Marehemu Samaahat Sheikh Abdallah Seifu (ra), ukarimu aliokuwa nao na jinsi gani alikuwa tayari kujitolea katika masuala ya kijamii.
Picha za tukio hilo ni kama ifuatavyo:
Maoni yako